Loading...
 

Uundaji wa Klabu- Kutafuta Mahali pa Mkutano

 

Kutafuta mahali pa mkutano.

(Hatua hizi zinahusu tu klabu ambazo zinakutana uso kwa uso)

Ukumbi wa mkutano unatakiwa kuwa na sifa zifuatazo: 

  • Uwe sehemu yenye faragha na ukimya.
  • Unatakiwa kumudu idadi ya watu ambao unawategemea, wakae kwa kustarehe.
  • Unatakiwa uwe na sehemu iliyotenganishwa ambao unaweza kutumiwa kama "jukwaa".
  • Mwanzoni, inatosha kama sehemu ina nafasi ya takribani watu 15 labda kama una uhakika kuwa watu zaidi watahudhuria.

 

Kitu kingine chochote ni nyongeza inayokaribishwa:

  • Runinga ambayo inaweza kuunganishwa na kompyuta, au (afadhali zaidi) projekta.
  • Mpangilio wa chumba (au ambao wamiliki wataruhusu upangiliwe) mpangilio wa "thieta"/"bwalo", "darasa" au "mtindo-u".
Thieta Darasa Umbo-U
Room 1 Room 2 Room 3

 

  • Jaribu kuepuka mpangilio wa mtindo "mkutano", "karamu", na "shimo mraba":
Mkutano Karamu Shimo Mraba
Room 6 Room 5 Room 4

 

  • Jaribu pia kuepuka mpangilio ambao hadhira hawajakaa kwa usawa kwenye maeneo mawili tofauti au zaidi au kuwa na vizuizi katikati ya hadhira na eneo la mzungumzaji:
Tofauti ya Usawa wa Hadhira Vizuizi
Room 7 Room 8
  • Kama unaweza, jaribu kuweka mlango wa kuingilia uwe mbali iwezekanavyo na eneo la mzungumzaji ili kuepuka usumbufu kama mtu akiingia au akiondoka kwenye chumba wakati wa mkutano.
Mlango kwa nyuma Mlango kwa mbele
Room 9 Room 10

 

Wakati wa kutafuta ukumbi, weka akilini mikutano ambayo itakuwa na urefu wa masaa mawili (ili kuwa kwenye usalama).

Baadhi ya mawazo ya mahali pa mikutano:

  • Vyumba kwenye shule, vyuo vikuu, maktaba, au jengo lolote la umma. Kwasababu sisi ni shirika lisilo la faida, hatutozi ada yoyote na shughuli zetu na mikutano ina asili ya kielimu, taasisi hizi zinaweza zikatoa ukumbi bure. Kwa kawaida ni suala ambalo kila mtu anashinda: klabu inapata chumba cha mkutano ambacho kinaweza kutumia bure, na shule au chuo kinapata shughuli (na ambayo pia imeombwa) ambayo wanaweza wakawapa wanafunzi wake bila gharama na nguvu yoyote - hawajalipia kitu chochote au kuandaa au kutumia juhudi zozote.

    Kama unahitaji sisi kuandika barua rasmi kwenda kwa taasisi ya serikali au umma ili kuthibitisha kuwa sisi ni shirika lisilo na faida na unataka kupata chumba, tunaweza kufanya hivyo. Tafadhali tuandikie kwenda info@agoraspeakers.org. Tafadhali toa taarifa za taasisi (anuani kamili) na jina lake, barua pepe, na nafasi ya mtu ambaye unataka sisi tumuandikie.

    Tafadhali tambua kuwa tunaweza kutoa barua rasmi za msaada kwa lugha ya Kiingereza na Kihispania.
     
  • Kama ukiandaa muda wa mkutano kwenye siku inayofaa, migahawa au baa zinaweza zikawaachia mtumie chumba bure ilimradi wanaohudhuria wanunue, kwa mfano, kinywaji, au vinginevyo siku hiyo sehemu yao inaweza ikawa haina watu. Kwahiyo, wote mmeshinda: wamepata wateja, mmepata chumba cha faragha bure.
  • Baadhi ya watu ambao wamevutiwa wanaweza wakawa wanafanya kazi kwenye makampuni ambayo yanaweza yakawapa sehemu ya kukutana kwenye maeneo yao. 
  • Kama uanachama wa klabu ni mdogo, mnaweza hata mkakutana kwenye nyumba ya mtu mwingine.
  • Kama yote yakishindikana, unaweza ukakodi chumba kwa masaa mawili na mkagawana gharama kati ya watu waliohudhuria. Baadhi ya miji inatoa "anti-cafes" (kupinga migahawa), ambapo watu wanalipa kutokana na wanavyokaa na wanapata kufurahia vyumba vizuri, chai ya bure, nk.
  • Kama hamna uwezekano mwingine wowote ule na hali ya hewa inaruhusu, mnaweza mkakutana kwenye bustani. Mikutano hii ya nje mara nyingine inafanywa makusudi, hata na klabu ambazo zina ukumbi mzuri wa mkutano, inawatoa watu kwenye maeneo yao ya kustarehe na inavutia watu wengi kudadisi ambao baadae wanaweza kujiandikisha.

 

Mkutano wa wazi wa klabu wa Parlanchines mjini Madrid, kwenye bustani ya Retiro.
Mkutano wa wazi wa klabu wa Parlanchines mjini Madrid, kwenye bustani ya Retiro.

 

Kumbuka kuwa haupo pekee yako na hauuzi bidhaa au huduma na haushughuliki na "wateja", lakini badala yake, unatengeneza mazingira ambayo yatasaidia watu wengine kwenye maisha yao. Washughulishe watu wote wanaotaka kwenye kutafuta ukumbi. Unaweza ukapata mawazo na mapendekezo ambayo haukuyafikiria.

 

Kwa mkutano wa kwanza, jaribu gharama za kuanzia ziwe chini iwezekanavyo.


Contributors to this page: zahra.ak and agora .
Page last modified on Wednesday June 2, 2021 16:17:48 CEST by zahra.ak.